STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 23, 2016

Ronaldo azinduka, Ureno yapenya 16 Bora, Ufaransa, Ireland kimbembe

ronaldo.jpg
Ronaldom akishangilia moja ya mabao yake ya usiku wa kuamkia leo yaliyoibeba Ureno kuambulia sare na kutinga 16 Bora
CRISTIANO Ronaldo ameondoa gundu kwa kuifungia timu yake mabao mawili wakati Ureno ikisaka sare ya tatu mfululizo katika mechi zake za Kundi F za michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016) dhidi ya Hungary.
Timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 3-3, huku Ureno kupitia Ronaldo wakilazimika kusawazisha mara zote kuambulia pointi iliyowabeba kama mshindwa bora.
Sare hiyo imeisaidia Ureno kuingia hatua ya mtoano ya 16 Bora kama mshindi wa tatu na sasa itakutana na Croatia katika mechi itakayopigwa Jumamosi hii.
Iceland inayoshiriki kwa mara ya kwanza imendelea kufanya maajabu kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Austria na kusonga mbele kama mshindi wa pili wa kundi hilo wakilingana pointi na vinara Hungary.
Italia nayo ilipoteza mechi yake ya mwisho dhidi ya Ireland nma Belgium ikaizabua Sweden bao 1-0 na kumtia aibu Zlatan Ibrahimovic ambaye amestaafu timu hiyo akishindwa kuifungia timu yake bao lolote katika fainali hizo za Euro 2016. Sweden imeaga michuano hiyo ikiwa ina pointi moja na bao moja la kufunga.
Kwa mujibu wa ratiba ya hatua hiyo ya 16 Bora, wenyeji Ufaransa watavaana na Ireland na kukumbushia tukio la mwaka 2010 wakati Thierry Henry alipoivusha timu yake kwa bao la mkono dhidi na wapinzani wao hao.
Ratiba kamili ya 16 Bora ipo hivi:
Juni 25, 2016
Uswisi  v    Poland       
Wales    v   Ireland ya Kaskazini
Croatia v    Ureno

Juni 26, 2016
Ufaransa    v Ireland       
Ujerumani v Slovakia
Hungary    v Belgium       

Juni 27, 2016
Italia      v Hispania
England v Iceland

No comments:

Post a Comment