STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 23, 2016

Copa America 2016 ni Chile na Argentina tena

Fun and games in Chicago. 
https://heavyeditorial.files.wordpress.com/2016/06/gettyimages-542227446.jpg?quality=65&strip=all&strip=allCHILE imetinga fainali za Copa America kwa mara ya pili mfululizo na watavaana na Argentina katiak mechi inayorejea fainali za mwaka jana ambapo ilibeba taji kwa ushindi wa bao 1-0.
Watetezi hao walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Colombia katika mechi ya Nusu Fainali iliyosimama kwa muda wa saa mbili kutokana na hali mbaya ya hewa ya jiji la Chicago lililotumiwa kwa mchezo huo mkali.
Mabao ya mapema ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Charles Aranguiz aliyefunga dakika ya 7 na jingine la Jose Fuenzalida aliyetumbukiza kimiani dakika 11 yalitosha kwa Chile kutinga fainali na sasa itavaana na Argentina iliyotangulia mapema jana.
Argentina iliisasambua wenyeji Marekani kwa kuicapa mabao 4-0, huku nahodha Lionel Messi akifunga bao la tatu lililomfanya aweke rekodi ya kuwa Mfungaji Bora wa muda wote wa taifa hilo akifikisha bao la 55 na kuipiku rekodi ya Gabriel Batistuta aliye na mabao 54.
Katika fainali zilizopita Argentina ilikubali kipigo cha mkwaju ya penalti 4-1 na kuwapa wenyeji Chile taji lao la kwanza katika historia ya michuano hiyo iliyoasisiwa miaka 100 iliyopita (1916).
Pambano hilo la fainali za mwaka huu zitachezwa Jumapili kwenye Uwanja wa
MetLife, East Rutherford ambapo pia mbali na mataifa hayo kusaka ubingwa pia zitakuwa katika vita ya nyota wao, Eduardo Vargas wa Chile mwenye mabao 6 na Messi mwenye mabao matano watakaokuwa wakiwania Kiatu cha Dhahabu
.

No comments:

Post a Comment