STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 23, 2016

Chelsea yammezea mate Koulibaly wa Napoli,

http://img.20mn.fr/txPrUEwrTRCJig7saa8abQ/2048x1536-fit_kalidou-koulibaly-lors-lazio-naples-18-janvier-2015.jpg
Kalidou Koulibaly
IKIJIANDAA kumpokea Kocha wake mpya, Antonio Conte, klabu ya Chelsea imedaiwa ipo kwenye mawindo dhidi ya beki wa Napoli, Kalidou Koulibaly ikitoa  ofa ya Pauni Milioni 19.2.
Chelsea imekuwa ikimzimia kupita kiasi beki huyo wa kimataifa wa Senegal, ambaye ameingia katika mzozo na klabu yake kuhusiana na uhamisho wake.
Licha ya mzozo huo, tayari kuna taarifa kwamba ofa hiyo ya Chelsea imeshakataliwa na Napoli ikidaiwa inataka kitita cha Pauni Milioni 30, ili imuachie nyota huyo mwenye umri wa miaka 24.
Klabu ya Napoli ilichukizwa na Koulibaly kufuatia madai aliyotoa kuwa yuko tayari kuzungumza na Chelsea.
Beki huyo alisema hajazungumza na Kocha Antonio Conte, lakini anadhani hilo litafanyika hivi karibuni, baada ya kumaliza majukumu yake ya Euro akiiongoza timu ya taifa ya Italia iliyotinga hatua ya 16 Bora kwa sasa nchini Ufaransa

No comments:

Post a Comment