MAELFU ya watu
wanatarajiwa kumuaga aliyekuwa bondia shupavu Muhammad Ali nyumbani
kwake katika mji wa Louisville huko Kentucky.![]() |
Muingizaji Will Smith na aliyekuwa bondia Lenox Lewis watakuwa miongoni mwa wale watakaobeba jeneza lake ,huku aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton akitarajiwa kutoa hotuba.
![]() |
![]() |
| Muhammad Ali enzi za uhai wake siku za karibuni |
Rais Obama hatakuwepo,kwa kuwa anatarajiwa kuhudhuria sherehe ya kufuzu kwa mahafala ya mwanawe mkubwa Malia.Mshauri mkuu wa ikulu ya rais Valerie Jarret ambaye alimjua Ali atamwakilisha rais.

![]() |
| Nyumbani kwa marehemu |
Msomi wa Kiislamu Sherman Jackson alisema:Kufariki kwa Muhammad Ali kumetufanya tujisikie wapweke duniani.''Kitu kizima,kitu kikubwa na kinachovutia na kinachotoa uhakika wa maisha kimetuwacha''.

BBC




No comments:
Post a Comment