STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 22, 2010

Masilahi ya Ubunge ndio chanzo cha watu kuchafuana-Chayeka



MASILAHI makubwa wanayolipwa na kuyapata Wabunge, yanaelezwa ndio chanzo cha mfarakano miongoni mwa wana CCm kiasi cha kufikia kuchafuana wakipakaziana masuala ya utata wa uraia na mambo mengine yakudhalilishana.
Hayo yamesemwa na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya wa Tarime, Raphael Chayeka, alipozungumza na Micharazo wilayani Kilosa, ambapo alisema masilahi manono wanayolipwa wabunge ndiyo yanayofanya kila mmoja kupigana kufa na kupona kuona anakuwa mbunge.
Chayeka alisema hali hiyo ya tamaa na uchu iliyowanayo watu wengi wanaojitosa kwenye siasa ndio wanaopelekea wanaoangushwa kuwachafua wenzao kwa minajili ya kuona wanapata nafasi ya kuteuliwa, kitu alichodai sio uungwana katika dunia ya wastaarabu.
Alisema donge nono la kwenye masuala ya ubunge na siasa kwa ujumla ndiyo inayofanya kila mtu sasa bila kujali wa kada gani kutaka kuwa mwanasiasa na hasa ubunge na pale wanaposhindwa kwenye kura ndipo wanapoibuka kuwachafua wengine.
"Masilahi manono yaliyopo kwenye Ubunge na Siasa kwa ujumla ndio yanayopelekea watu kuchafuana na kupakaziana mambo mabaya, lakini kama sio hivyo wala yasingetokea hayo yaliyojitokeza miaka ya hivi karibuni," alisema Chayeka.
Naye Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilosa, Alhaj Shaweji Abdallah naye alisema ifike wakati wanachama wa CCM na wagombea wengine wawe waungwana kwa kubali matokeo badala ya kuwapakazia wenzao masuala ambayo yanayowadhalilisha wengine bila sababu ya msingi.
Wazee hao walitoa kauli hizo wakati wakimtetea mgombea ubunge wa jimbo la Kilosa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo aliyevumishiwa kuwa sio raia wa Tanzania bali ni mtu wa Malawi kitu kilichomshangaza waziri mwenyewe kwa madai anatambue yeye ni raia.

Mwisho

No comments:

Post a Comment