STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 23, 2013

Kinyambe aufungua mwaka na mpya

KInyambe akiwa katika pozi zake
MCHEKESHAJI anayezidi kutamba nchini kwa sasa, Mohammed Abdallah 'Kinyambe' ameufungua mwaka 2013 kwa kuachia filamu yake mpya iitwayo 'Urithi wa Kinyambe'.
Akizungunza na gazeti hili, Kinyambe anayefahamika pia kama James, alisema filamu hiyo tayari imeshaingia sokoni akiwa ameigiza na wasanii kadhaa maarufu nchini.
Kinyambe mwenyeji wa Mbeya, alisema baadhi ya wasanii alioigiza nao filamu hiyo ya vichekesho ni pamoja na Chrispin Masele 'Masele Chapombe' na Erick Ivyoivyo.
"Nimeuanza mwaka mpya kwa kuachia sokoni filamu yangu mpya ya komedi iitwayo 'Urithi wa Kinyambe' ambayo nimeigiza na wakali kadhaa akiwemo Masele na Erick Ivyo ivyo ninaotamba nao kwenye 'Vituko Show'," alisema Kinyambe.
Kinyambe alisema kazi hiyo mpya ni mwanzo wa raha alizojiandaa kuwapa mashabiki wake, kwani pia anajipanga kuwapa burudani katika muziki.
"Mashabiki wangu wakae tayari kupata vitu vizuri, kwani baada ya Urithi wa Kinyambe pia nakamilisha nyimbo zangu kadhaa ili niikamilishe albamu yangu," alisema.
Msanii huyo, alisema nyimbo mpya hizo zinakuja baada ya kuachia vibao vitatu tofauti kama 'Maumivu' alioimba na Baguje, 'Maimuna' alioimba na Leila Tot na Erick Ivyo ivyo na kile cha 'Kiduku Mpapaso' aliomshirikisha Kesse.

1 comment: