STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 23, 2013

Masilahi yampeleka Kambi Msondo Ngoma

Muimbaji Athuman Kambi (wa pili toka kulia) akiwa na waimbaji wenzake wa Msondo Ngoma. Kutoka Kushoto ni Hassan Moshi , Eddo Sanga na Juma Katundu

MWANAMUZIKI mpya wa bendi ya Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki', Athuman Kambi amesema kusaka masilahi na kujifunza zaidi muziki ndiko kulikomhamisha kutoka Mlimani Park 'Sikinde'.
Aidha muimbaji huyo anayeshabihiana sauti na mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Hassani Rehani Bitchuka, amewaomba mashabiki wa Msondo kuwa na subira kabla ya kupata vitu adimu kutoka kwake.
Akizungumza na MICHARAZO, Kambi alisema hakuna kitu chochote kilichomtoa Sikinde na kutua Msondo zaidi ya kutafuta masilahi zaidi na pia kujifunza kwa wakongwe waliopo ndani ya bendi hiyo mpya aliyonayo.
Kambi alisema ameondoka Sikinde kwa amani na urafiki bila kugombana na mtu yeyote na kwamba hata kama mambo yatamshinda Msondo iwe rahisi kwake kurejea katika bendi hiyo iliyomtangaza hasa kwa kuweza kuimba kwa ufasaha sauti ya Bitchuka.
"Sijaondoka kwa ugomvi Sikinde, kilichonipeleka Msondo mbali na kusaka masilahi zaidi, lakini naamini nitaongeza ujuzi kwa kujifunza kutokwa wanamuziki waliopo ndani ya bendi hiyo," alisema.
Kambi aliongeza hana cha kuwaahidi kwa sasa Msondo zaidi ya kuomba wampe muda aweze kujipanga ili kuwapa vitu adimu ambavyo hawajawahi kuvipata.
"Wanipe muda nizoee mazingira kisha waone nitawapa kitu gani, ila nimejipanga kuwapa fadhila kwa namna walivyonipokea," alisema.
Muimbaji huyo alijiunga na Msondo wiki mbili zilizopita na tayari ameshaanza mazoezi na kushiriki maonyesho ya bendi hiyo.
-------

No comments:

Post a Comment