STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 23, 2013

Arsene Wenger amvulia kofia Diame


LONDON, England
KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amemwagia sifa kiungo wa West Ham na ambaye wanamfukuzia kumnasa katika kipindi hikicha usajili wa dirisha dogo la Januari, Mohamed Diame.
Arsenal wamekuwa wakihusishwa mara kwa mara na usajili wa kiungo huyo mwenye miaka 25, anayeaminiwa kuwa na kipengele katika mkataba wake kinachomruhusu kuondoka ikiwa zitalipwa paundi za England milioni 3.5 (Sh. bilioni 9)
Diame ameonyesha kiwango cha juu na kuibuka kuwa mmoja wa wachezaji nyota wa klabu hiyo msimu huu, akifunga mabao mawili, yakiwamo dhidi ya Arsenal  katika mechi yake ya 18 tangu aanze kuichezea timu hiyo inayoongozwa na kocha Sam Allardyce.
Wenger ameongeza uvumi kuhusiana na kiungo huyo mwenye mwili 'jumba' wa timu ya taifa ya Senegal, akiwaambia waandishi wa habari: "Anafanya vitu vikubwa katika mechi, nimemuona akionyesha kiwango cha juu."
Arsenal ilifungwa 2-1 katika mechi yao dhidi ya Chelsea Jumapili, hivyo kuambulia pointi moja tu katika mechi tatu zilizopita za Ligi Kuu ya England ambazo zinawafanya waachwe kwa pointi saba na mahasimu wao katika kuwania nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, Tottenham na pia kulingana na Liverpool na West Brom ambao wote wana pointi 34.
Hata hivyo, kuna habari njema kwa Arsenal kufuatia taarifa za kupona kwa kiungo wao Mikel Arteta aliyekuwa nje kutokana na majeraha.

No comments:

Post a Comment