STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 26, 2013

RAGE AWASHUSHUA WANAOTAKA AJIUZULU


MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amewaumbua wale wote wanaomshinikiza ajiuzulu kufuatia mwenendo mbaya wa timu yao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, akidai hatajiuzulu ng'o kwa madai yeye siyo mchezaji wala kocha ndani ya Simba hivyo hapaswi kusakamwa.
Hata hivyo alifichua kitu gani kilichopo nyuma ya wanaomshinikiza ang'oke akidai ni tabia yake ya uwazi na msimamo wake dhidi ya rasilimali na mapato ya Simba ndiyo chanzo cha kuonekana mbaya, japo uongozi wake unatimiza wajibu wake kama unavyopaswa katika kuhakikisha kila kitu kinaenda vema Msimbazi.
Rage alitoa msimamo huo jana alipozungumza na waandishi wa habari na kukuanusha taarifa kwamba huenda angeachia ngazi na badala yake alisema yeye bado yupo sana Simba, ingawa alisisitiza kuwa kamati ya utendaji ya klabu hiyo itakutana ili kujadili kinachoendelea ndani ya Simba.
Alisema maamuzi ya kamati hiyo huenda yaakatoka na maamuzi magumu na atayatangaza mbele ya mkutano wa wanachama atakaoutisha kuwapa kila kitu kinachoendelea ndani ya Simba kwa sasa na kuifanya timu yao kwenda kwa kusuasua katika ligi kuu.
"Wanaotaka mie nijiuzulu niwaulie mie nacheza namba ngapi au mie ni kocha?...Mimi ni mwenyekiti na wajibu wangu kuhakikisha timu inapata kila linalohitajika, kwa mfano hivi sasa Simba inatakiwa kwenda Angola kurudiana na Libolo ni wajibu wangu kuisafirisha klabu iwe na fedha au la, watu wabadilike," alisema.
Aliongeza, uwazi wake katika udfhibiti wa mapato na vitega uchumi vingine vya Simba ndiyo uliomtengenezea maadui, ila akahoji mbona wanachjama wanaomshikiniza kujiuzulu hawajawahi kuhoji zilipo fedha za wachezaji waliouzwa Ulaya kama akina Haruna Moshi 'Boban', Henry Joseph kama uongozi wao ulivyoweka kila kitu hadharani ilipowauza akina Mbwana Samatta, Patrick Ochan na sasa Emmanuel Okwi.
Juzi mara baada ya pambano la Simba na Mtibwa Sugar ambapo 'Mnyama' alilala kwa bao 1-0, kulikuwa na tetesi kwamba Rage alikuwa akijiandaa kujiuzulu kwa kuhisi anahujumiwa na watu ili aonekane hafai.

No comments:

Post a Comment