STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 23, 2013

African Lyon kujishusha daraja kesho kwa JKT Ruvu?

 
African Lyon

JKT Ruvu

Na Boniface Wambura
LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itaendelea tena kesho (Aprili 24 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya wenyeji African Lyon dhidi ya maafande wa JKT Ruvu.
Mechi hiyo namba 165 itachezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Kamishna Hamisi Kisiwa wa Dar es Salaam. Waamuzi wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Hashim Abdallah, Omari Kambangwa, Abdallah Selega na Said Ndege wote wa Dar es Salaam.
Lyon inahitajika kushinda pambano hilo angalau kufufua matumaini ya kusalia msimu ujao ujao, lakini matokeo yoyote kinyume na ushindi ni kujitia muhuri wa kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Timu hiyo inayoburuza mkia wa msimamo wa ligi hiyo na pointi 19 tu ikilingana na Polisi Moro, na ushindi pekee ndiyo utawaondoa kwenye janga la kurudi 'mchangani'.
Hata hivyo JKT Ruvu wanaouguza kipigo cha mabao 3-0 toka kwa vinara wa ligi hiyo, Yanga nayo haipo katika nafasi nzuri na kupoteza mchezo wa kesho itamaanisha kwamba nao wanajiweka kuelekea kwenye FDL.
Maafande hao wana pointi 23 na wamesaliwa na mechi tatu, hivyo matokeo yoyote mabaya kwao yataweka bapaya kama ilivyo kwa Lyon na hivyo kufanya pambano hilo kuwa kama vita baada ya 'wanyonge' hao wawili waliopo maeneo ya mkiani.

No comments:

Post a Comment