STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 25, 2013

Ally Mustafa 'Barthez' afichua siri nzito Yanga

Kipa Ally Mustafa 'Barthez' akiwa mazoezini

KIPA tegemeo wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ally Mustafa 'Barthez' amefichua siri akidai kung'ara kwake katika msimu wa kwanza ndani ya Yanga kumetokana na kuaminiwa na makocha pamoja na kuungwa mkono na wachezaji wenzake, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.
Barthez aliyeitwa kwenye kikosi cha pili cha timu ya taifa 'Young Taifa Stars', alisema pia kiu kubwa ya mafanikio aliyokuwa nayo na kutaka kuwadhihirishia Watanzania kwamba yeye ni mkali ndiyo iliyomfanya kujituma zaidi na kuipigania Yanga kufanya ilivyofanya msimu huu.
Akizungumza na MICHARAZO, Barthez aliyetua Yanga akitokea Simba alikokuwa akisugua benchi nyuma ya kipa Juma Kaseja, alisema ameweza kung'ara kwa sababu makocha aliokutana nao Jangwani walimuamini na kumpa nafasi ya kuonyesha kipaji alichonacho.
Barthez, alisema ni vigumu kwa mchezaji yeyeote kuweza kuonyesha ubora wake kama hapewi nafasi na hata yeye hakuonekana bora mahali alipotoka kwa vile hakuamini na kupewa nafasi ya kucheza tofauti na tangu atue Yanga.
"Najisikia faraja kufanikiwa kuisaidia Yanga, pia kurejesha heshima yangu, lakini hii haikuja kimiujiza bali ni kutokana na makocha wangu kuniamini na kunipa nafasi sambamba na ushirikiano mzuri ninaopata kwa wachezaji wenzangu na sapoti kubwa ya wanachama na mashabiki," alisema.
Kipa huyo aliyewahi kutamba na timu mbalimbali za wilayani Ilala kabla ya kupanda daraja na Ashanti United kisha kunyakuliwa na Simba mwaka 2005, alisema bado hajaridhika na mafanikio aliyonayo akiota kuisaidia zaidi Yanga na hasa kwenye michuano ya kimataifa.
Barthez aliyetua Yanga na mguu mzuri kwa kuiwezesha kuibebesha taji la Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo Julai mwaka huu kisha kukaribia kuipa taji la 23 la Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema anatambua changamoto inayomkabili kuendelea kubaki kuwa bora na atajituma zaidi.

No comments:

Post a Comment