STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 25, 2013

Lewandowski ainyanyasa Real Madrid Ligi ya Ulaya

Robert Lewandowski aliyeiua Real Madrid jana usiku
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski usiku wa jana aliinyanyasa atakavyo Real Madrid baada ya kuwatungua mabao manne na kuiwezesha klabu yake ya Borussia Dortmund kuizabua timu hiyo ya Hispania kwa mabao 4-0 katika pambano la Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lewandowski aliyefunga bao mopja kipindi cha kwanza na mengine kipindi cha pili, ameiweka mabingwa wao zamani wa Ulaya kutoka Ujerumani ambao hivi karibuni walitemesha taji la Bundesliga, katika nafasi nzuri ya kufuzu fainali.
Mkali huyo anayefukuziwa na klabu mbalimbali za Ulaya ikiwamo Manchester United, alifunga bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya nyota wa Madrid, Cristiano Ronaldo kusawazisha bao dakika mbili kabla ya mapumziko.
Akiwainyanyasa atakavyo ngome ya Madrid, Lewandowski alifunga mabao mawili ndani ya dakika tano mara baada ya kipindi cha pili kuanza akifunga la pili dakika ya 50 na kuongeza jingine dakika ya 55 kabla yua kumalizia udhia dakika ya 67 kwa bao la penati.
Kipigo hicho kimeiacha Madrid wakiwa hoi wakisubiri miujiza kupitia kocha wao Mreno Jose Mourinho kusaka ushindi katika mechi ya marudianoi itakayochezwa wiki ijayo nyumbani kwao ili kufuzu fainali wakihitajika kushinda mabao 3-0.
Pia kipigo hicho cha Madrid jana kimeongeza machunbgu ya Wahispania ambao walikuwa wakiota kushuhudia fainali ya El Classico Mei 25 kufuatia Barcelona juzi kugaragazwa na mabingwa wa Ujerumani na wanafainali wa mara tatu katika miaka miaka minne Bayern Munich kwea mabao 4-0 na kufifisha matumaini hayo.

No comments:

Post a Comment