STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 25, 2013

Hii kali! Sherehe za Muungano zakwamisha pambano la Simba na Ruvu Shooting Taifa

 
Viongozi wakuu wa TFF, Leodger Tenga na Angetile Osiah
Na Boniface Wambura
PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeahirishwa mpaka Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

Kisa cha kufanyika ghafla kwa mabadiliko ya pambano hilo imetokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.

Kitendo hicho cha mechi hiyo kuahirishwa ghafla kinauonyesha umuhimu wa klabu na hata FA kumiliki uwanja wake ili kuondokana na matatizo kama hayo yanayolitia doa soka la Tanzania.

Hata hivyo pamoja na pambano hilo kupigwa 'dochi' hadi Mei 5, TFF imesisitiza kuwa ratiba nyingine za ligi hiyo inayopelekea ukingoni itaendelea kama ilivyo, ambapo kesho (Aprili 26 mwaka huu) Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Jumapili 'Mnyama' Simba itaikaribisha Polisi Moro kwenye pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa siku ya Jumapili (Aprili 28 mwaka huu).

No comments:

Post a Comment