Baadhi ya wachezaji wa timu ya Golden Bush Veterani |
TIMU za soka za Golden Bush Fc inayoshiriki Ligi Daraja la Nne wilaya ya Kinondoni na Golden Bush Veterani asubuhi ya kesho zinatarajiwa kumenyana katika pambano la kirafiki huku wakishuhudiwa na wakala wa soka kutoka Msumbiji, Ashraf ambaye atakuwa na kazi ya kuangalia vijana wa kuondoka nao.
Kwa mujibu wa msemaji na mlezi wa timu hizo Onesmo Waziri 'Ticotico' pambano hilo litachezwa saa 1:30 asubuhi kwenye uwanja wa Kinesi maarufu kama St James Park, huku wakala huyo aliyekuwa kusaka wachezaji wa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini kwao atakuwa na akishuhudia pambano hilo.
Ticotico alisema tayari mmoja wa wachezaji wa kikosi cha vijana wanaoongoza kwenye msimamo wa kundi lao katika ligi wanayoshiriki wakiwa na pointi 12 kwa michezo minne bila kupoteza wala kutoa sare mechi yoyote, lakini alikuwa akipenda kuwaangalia vijana vizuri kabla ya kuondoka na vijana watakaomkuna kisoka.
"Kesho
uwanja wa Kinesi (st James park) utakuwa moto ambapo timu hizo mbili
zitaumana kuanzia saa moja na robo asubuhi. Game hii itakuwa kipimo
tosha kwa wazee ambao watakuwa wanafanya maandilizi ya mwisho kabla ya
bonanza la Pugu siku ya jumapili week hii ambapo Golden Bush tumepata
mwaliko maalum na Mbunge wa Ukonga Mama Mwaiposa," alisema.
Ticotico alisema pambano hilo litachezeshwa na mwamuzi Fred Mazuni badala ya waamuzi waliozoeleka katika mechi za timu hizo, Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' au Ally Mayay.
Ticotico alisema pambano hilo litachezeshwa na mwamuzi Fred Mazuni badala ya waamuzi waliozoeleka katika mechi za timu hizo, Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' au Ally Mayay.
Katika mechi mbili baina ya timu hizo Wazee walinyanyaswa kwa vipigo mfululizo, jambo ambalo ndilo limefanya abadilishwe mwamuzi kwa hisia kwamba Babu Mada na Mayay wamekuwa wakiibeba timu ya vijana ambao ni viongozi na makocha wao.
No comments:
Post a Comment