Katibu Mkuu wa chama hicho, Abeid Kasabalala alisema tuzo hizo zitatolewa kwa mwanasoka bora wa mwaka, mwanasoka bora chipukizi, kocha bora wa msimu na kipa bora.
Alisema tuzo hizo zinazodhaminiwa na Kampuni ya Kishen Enterprises Ltd zitakuwa zikitolewa kila mwaka kuwaongezea wachezaji ari uwanjani wakati wa mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
“Makocha na viongozi kutoka mikoa mbalimbali wanatarajia kuwasili kesho (leo) ambao kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya Sputanza, watafanya uteuzi wa washindi kwa kutumia vigezo vilivyopo,” alisema Kasabalala.
Aliongeza kuwa katika tuzo hizo, pia watatoa vyeti vya kuwakumbuka na kuwapongeza wachezaji wa zamani waliochezea timu ya taifa miaka ya nyuma ambapo alisema kiingilio kitakuwa sh 10,000 na sh 50,000.
No comments:
Post a Comment