STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 21, 2013

Kocha Patrick Liewig aipa Simba siku 4

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2012/12/Patrick-Liewig.jpg
Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig
ALIYEKUWA kocha mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Liewig, ameipa klabu hiyo siku nne kuhakikisha kuwa wanamlipa madai yake kabla hajamtaka mwanasheria wake kuwashtaki ifikapo Jumatatu.
Liewig aliyechukua mikoba ya kuifundisha Simba baada ya Mserbia Milovan Cirkovic, aliliambia gazeti hili kuwa anadai kiasi cha dola za Marekani 26,000 (Sh. milioni 42).
Akizungumza na NIPASHE jana, Liewig, alisema kwamba amemueleza Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hanspoppe Zacharia, kuwa anahitaji kupewa haki yake hiyo ili arejee kwao na hapendi kuona anabaki nchini wakati hana kazi.
Liewig alisema kuwa anashangazwa kuona Simba wakishindwa kumpa taarifa za kusitishwa kwa mkataba wake kwa maandishi na kumuacha arejee nchini.
"Nilianza kusikia kwamba Simba hainihitaji mapema, hata waandishi walipenda kuniuliza hatma yangu kila mara Simba ilipokuwa inapoteza mechi... kumbe walitaka niamke na kujua kuwa nafasi yangu ndani ya klabu ni ndogo," alisema kocha huyo.
Aliongeza kuwa hivi sasa anasubiri kukutana na Hanspoppe ili ajue malipo yake yatakavyokuwa na haamini hata kidogo kuwa klabu hiyo itatekeleza madai yake baada ya kuondoka nchini.
"Napenda haki zangu nizipate sasa ili tumalizane kwa amani. Si tabia njema kufikisha malalamiko CAF (Shirikisho la Soka la Afrika) au FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa)," aliongeza kocha huyo.
Simba iliamua kuachana na Liewig baada ya timu yake kushindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mwishowe kumrejesha kocha na mchezaji wao wa zamani, Abdallah Kibaden 'King'.
Hata hivyo, ni uongozi wa Simba ndiyo uliokuwa ukiunga mkono uamuzi wa kutowachezesha baadhi ya nyota wao wenye majina makubwa kama Haruna Moshi 'Boban' na Juma Nyosso na kuwachezesha zaidi yosso wao kuelekea mwishoni mwa msimu na mwishowe kujikuta wakipoteza ubingwa mapema.
Liewig anaidai Simba fedha za mshahara wake wa mwezi Aprili na Mei mwaka huu ambao ni dola za Marekani 14,000 (Sh. milioni 14) na kingine kilichobakia kinatokana na makubaliano ya kuvunja mkataba wao uliopaswa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Hanspoppe alikiri kuwa Simba inadaiwa na kocha huyo na kueleza kwamba klabu inasaka fedha kutoka kwa wadau wake ili kuhakikisha wanalipa madeni yote kabla ya kuanza kwa msimu mpya .
Mapema mwaka hii mmoja wa wanachama wa Simba, Rahma Al Kharoos, aliokoa jahazi kwa kumlipa Milovan madai yake baada ya kutimuliwa kama ilivyo sasa kwa Liewig.

Chanzo:NIPASHE

No comments:

Post a Comment