STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 6, 2013

MSD yatataka uwekezaji zaidi sekta ya dawa

BOHARI ya Dawa nchini (MSD) imetoa rai kwa wawekezaji kuwekeza katika sekta ya viwanda vya kuzalisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ili kuhakikischa kuwa nchi inapiga hatua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Isaya Mzoro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana na ukweli kuwa asilimia 80 ya dawa, asilimia 95 ya vifaa tiba na vitendanishi vya maabara asilimia 100 huagizwa kutoka nje hali ambayo inachangia fedha nyingi kufaidisha nchi zingine.
Mzoro alisema ni vema wawekezaji wan je na ndani wakajitokeza kuwekeza katika viwanda ambavyo vitajihusisha na uzalishaji wa mahitaji yote ambayo yanahusu afya ya binadamu hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kabla ya kuanzishwa MSD hapa nchini kulikuwa na viwanda vya kutengeneza dawa zaidi ya saba lakini hadi sasa ni viwanda viwili ambavyo vinafanyan kazi hivyo kusababisha Serikali kuagiza dawa kutoka nje.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba watu kutoka nje au ndani ya nchi kuwekeza katika sekta hii ya uzalishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwani ni fedha nyingi ambazo zinaenda nje kwa lengo hilo,” alisema.
Aidha alisema pamoja na changamoto hiyo kubwa ya ukosefu wa viwanda MSD imefanikiwa kufikisha huduma za ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa huduma zao kwa asilimia 75 jambo ambalo linawapa matumaini kwa siku za karibuni.
Mzoro alisema MSD kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali ina mpango wa kupanua maghala kwa kukamilisha ujenzi wa awamu ya pili ili kuongeza nafasi za kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
Alisema MSD inatumia mfumo wa EPICOR 9 tangu mwezi Agosti 2012 ambapo wanatoa mafunzo endelevu kwa watumishi wao ili waweze kutoa huduma kwa haraka na kwa ufanisi.
Kwa upande mwingine Kaimu Mkurugenzi huyo alisema MSD inakabiliwa na changamoto nyingi kama ongezeko kubwa la mahitaji ya dawa ukilinganisha na uwezo serekali, ucheleweshaji wa kufikishwa pesa MSD kutoka hazina, Halmashauri kutotumia vyanzo vingine vya fedha, uhaba wa viwanda vya dawa nchini.
Changamoto nyingine taratibu za ununuzi kuchukua muda mrefu na baadhi ya zahanati na vituo vya afya kutopeleka maombi ya dawa na vifaa tiba katika kanda za MSD kama utaratibu unavyohitaji.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema matarajio yao ni kushirikisha sekta binafsi katika kusambaza dawa na vifaa tiba, kubandika orodha ya dawa na vifaa tiba vilivyokabidhiwa vituoni, kuendelea kuweka nembo ya serikali kwenye vidonge, kushirikisha sekta binafsi katika kutoa huduma ya dawa na vifaa tiba na waganga kuwasilisha maombi mapema.

No comments:

Post a Comment