Peter Msechu |
Na Elizabeth John
HATIMAYE ngoma inayokwenda kwa jina
la ‘Kibudu’ liyoimbwa na mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Peter Msechu, imeanza
kutamba katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na ujumbe wa mashairi
yaliyomo ndani yake.
Mbali ya kutamba na kibao hicho,
mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Relax’, ‘Kumbe’ ambavyo
vilifanya vizuri zaidi mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vilimtambulisha
katika tasnia ya muziki huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Msechu alisema katika kazi hiyo kamshirikisha mkali wa muziki huo, Ally Nipishe
na kwamba tayari imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Alisema kibao hicho kakitengeneza
katika studio ya Ufundi Production chini ya mtayarishaji wake mahiri, Fundi
Samuel.
“Naomba mashabiki wangu wakipokee
vizuri kibao hicho ambacho natarajia kukifanyia video yake Nairobi, Kenya,”
alisema.
Msechu aliwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya video hiyo ambayo anatarajia kuitoa mwinzoni mwa mwezi ujao ikiwa ni pamoja na nyimbo nyingine nyingi zinazofuata.
No comments:
Post a Comment