Zuwena Mohammed 'Shilole' |
Akizungumza na MICHARAZO leo, Shilole alisema video hiyo iliyorekodiwa nchini Marekani alipoenda ziarani hivi karibuni kwa sasa inahaririwa kabla ya kuachiwa hewani mashabiki waone namna anavyokomaa na jiji.
Shilole alisema tofauti na nyimbo za nyuma kama 'Lawama', ' Dada Dume', 'Dudu' au 'Paka la Baa' ambazo zipo katika miondoko ya 'Chakacha' safari hii ametoka kivingine katika Bongofleva kuonyesha uwezo alionao katika fani hiyo ya muziki.
"Wakati wimbo wangu wa 'Nakomaa na Jiji' ukiendelea kuwa gumzo kwa sasa, nakamilisha mipango ya kuachia video yake hivi karibuni ili kuwapa raha mashabiki wangu," alisema Shilole.
Mkali huyo, alisema video hiyo aliipiga katika jiji la New York alipoenda Marekani na kwamba kila kitu kimekamilisha kwa ajili ya kuhakikisha anaiachia mapema iwezekanavyo.
Pia alisema kutoka hadharani kwa video ya 'Nakomaa na Jiji' itakuwa fursa yake nyingine ya kujiandaa kutoa kazi nyingine katika mtindo wa 'bandika bandua' ili kuwapa raha mashabiki wake.
Shilole alisema ana hazina kubwa ya muziki katika stoo yake na ndiyo maana kila mara anawaangushia mashabiki wake nyimbo mpya kali kama alivyofanya katika kazi zilizopita ambapo kabla ya 'Nakomaa na Jiji' alikuwa gumzo na wimbo wa 'Paka wa Baa'.
No comments:
Post a Comment