Na Suleiman Msuya
KWA kipindi cha zaidi ya miaka sita tangu kuanzishwa
kwa Baraza la Ushindani (FCT) jumla ya rufaa 84 zimesajiliwa 36 zimesikilizwa
na kutolewa uamuzi na jopo la wajumbe waa Baraza hilo.
Hayo yamebainishwa Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya
Uchumi wa FCT Nzinyangwa Mchany wakati akijibu swali la mwandishi wqa habari
hii leo jijini Dar es Salaam.
Alisema katika rufaa hizo 29 zilisitishwa kutokana
na wahusika kuamua kuziondoa baada ya kufikia maamuzi ambayo baraza hilo halina
mamlaka yakuingilia ambapo kwa sasa rufaa zinazoendelea kusikilizwa ni 19.
Mchany alisema Baraza la Ushindani limejipangia
kusikiliza rufaa 24 kwa mwaka iwapo zitakuwepo lakini bado mwitikio ni mdogo
hali ambayo inatajwa kuwa inachangiwa na uelewa mdogo kutoka katika jamii juu
ya FCT.
“Baraza la Ushindani FCT limeanza kazi rasmi mwaka
2007 ambapo huwa tunapokea rufaa kutoka katika kwa watu na taasisi mbalimbali
ambazo zinakuwa hazijaridhika na maamuzi ambayo yanatolewa na mamlaka za udhibiti hapa nchini,” alisema.
Kwa upande wake Mwanasheria Mwandamizi Hafsa Said alisema pamoja na mafanikio hayo madogo ambayo
wameweza kuyapata tangu kuanza kwa FCT bado wana changamoto chache ambazo
zinawakabili.
Alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni uchache wa
majaji wa kusikiliza rufaa ambapo wamekuwa wakifanya kazi kwa muda maalumu
(party time) kutokana na ukweli kuwa ni watumishi wa Mahakama ya Kuu nay a Rufaa.
Said alitaja changamoto nyingine ni ufahamu mdogo
kwa jamii juu ya FCT ambapo wanajipanga kwa kushirikiana na mamlaka za udhibiti
kutoa elimu hiyo ili wananchi na jamii kwa ujumla kutopoteza haki zao pale
wanapoona kuna dalili za kuzikosa.
Pia alisema pamoja na changamoto hizo kupitia
maamuzi yao wanayotoa ubora wa mamlaka za udhibiti umeongezeka jambo ambalo
linaleta tija kwa jamii.
Alisema tangu waanze kupokea rufaa zinazotoka kwa
taasisi na watu binafsi asilimia kubwa ya maamuzi yamekubalika ambapo ni
maamuzi mawili tu ndio yaliendelea katika ngazi zingine za kimaamuzi.
Mwanasheria huyo Mwandamizi alitoa wito kwa wananchi
na taasisi mbalimbali ambazo zinasimamiwa na mamlaka kama TCRA, SUMATRA, EWURA,
FCC na TCAA kujitokeza kukata rufaa iwapo watakuwa hawajaridhika na maamuzi
yao.
No comments:
Post a Comment