STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 22, 2013

Mmoja afa, wawili wakijeruhiwa kwa risasi



MTU mmoja amefariki baada ya kupigwa risasi kifuani na mwingine kujeruhiwa mikono yote miwili baada ya watu wasiojulikana kuwavamia na kutaka kuwapora mali huko Manyoni, Singida.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Igwamadete Kata ya Iseke Tarafa ya Nkonko wilayani humo baada ya mtu aliyejulikana kwa jina la Alody Joshua, 29 kupigwa risasi na majambazi hao.
 
Kadhalika Daudi Azaliwa amejeruhiwa mikono yote miwili baada ya kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakitoka kwenye mnada wa Mpapa kuelekea nyumbani ndipo majambazi hao walipoanza kuwapiga na kuwanyanganya fedha na kusababisha  kifo cha mtu huyo.

Jeshi la Polisi-Manyoni limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa watu watatu wanashilikiwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo na kwamba wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelzi kukamilika.
 
Chanzo Blog ya Singida.

No comments:

Post a Comment