STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 18, 2013

Chelsea yatupwa nje Capital One, Mkorea awanyamazisha, Man City haooo

Kitu Sundeland wakiizamisha Chelsea katika Capital One jana usiku
Edin Dzeko akiifungia Manchester City moja ya mabao yake mawili yaliyoivusha Nusu Fainali
BAO la muda wa nyongeza lililofungwa na nyota wa timu ya taifa ya Korea ya Kaskazini, Sung Yong Ki limeivusha 'vibonde' wa Ligi Kuu ya England Sunderland na kuizuia Chelsea kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Ligi 'Capital One'.
Sunderland inavuka hatua hiyo ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya muda mrefu na huku ikiwa katika hali mbaya kwenye ligi kuu, na sasa imeungana na Manchester City waliopata ushindi wa mabao 3-1 usiku wa jana katika mechi nyingine ya Robo Fainali ya michuano hiyo dhidi ya Leicester City.
Katika pambano la Sunderland waliokuwa nyumba dhidi ya vijana wa Jose Mourinho, dakika 90 ziliisha kwa timu hizo kufungana bao 1-1, Chelsea wakizawadiwa bao baada ya kiungo wa wenyeji, Lee Cattermole kujifunga dakika moja baada ya kipindi cha pili kuanza kabla ya Fabio Borini kusawazisha bao hilo dakika ya 88 ya mchezo huo uliokuwa ukionekana kama Chelsea wanaelekea kutinga Nusu Fainali.
Ndipo zikaongezwa dakika 30 za nyongeza na kushuhudia Chelsea wakishindwa kupata mabao mpaka dakika mbili kabla ya muda huo kumalizika Mkorea huyo kuifungia Sunderland bao lililowang'oa vijana wa Darajani nje ya michuano hiyo.
Katika pambano jingine Manchester City waliopo kwenye kiwango kwa sasa walipata ushindi ugenini wa mabao 3-1 na kutiunga nusu fainali dhidi ya wenyeji wao Leichester City.
Mpaka mapumziko wageni walikuwa na mabao 2-0 yaliyofungwa na Aleksandar Kolarov dakika ya 8 na Edin Dzeko aliongeza bao dakika ya 41.
Kipindi cha pili City waliongeza bao jingine dakika ya 53  kupitia tena kwa Dzeko akimalizia kazi ya james Millner kama ilivyokuwa kwa bao lake la kwanza na wenyeji kupata bao la kufutia machozi dakika ya 77 kupitia kwa  Lloyd Dyer.
Michuano hiyo itaendelea tena usiku wa leo kwa mechi nyingine za mwisho wa roboa fainali kati ya Manchester United itakayokuwa ugenini kuwakabili Stoke City na Tottenham kuikaribisha West Ham United.

No comments:

Post a Comment