STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 26, 2013

Liverpool vs Manchester City hapatoshi leo England

Nyota wa Liverpool, Luis Suarez ataendeleza makamuzi yake leo kwa Man City?

Wachezaji wa Manchester City watapongeza kama hivi leo mbele ya Liverpool au yatakuwa majanga?
LONDON, England
KIVUMBI cha Ligi Kuu ya England kinatarajiwa kuendelea leo ikiwa ni  Boxing Day kwa mechi 10 lakini pambano linalofuatiliwa kwa ukaribu ni lile la vinara, Liverpool na Manchester City ambazo msimu huu zimeonekana kuwa moto mkali.
Liverpool inayoongoza kileleni kwa tofauti na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa dhidi uya Arsenal zote zikiwa na pointi 36 itasafiri mpaka uwanja wa Itihad kuivaa Manchester City iliyopo nafasi ya tatu.
Man City imekuwa ikishinda kwa asilimia 100 kwenuye uwanja huo, huku Liverpool ikionyesha inagawa dozi nyumbanbi na ugenini kitu kinacholeta msisimko mkubwa kwa pambano hilo la leo.
Pointi mbili tu zinazozitofautisha timu zilizo tano bora, na leo timu inayoshika nafasi ya pili Arsenal itakuwa na kibarua ugenini dhidi ya West Ham, wakati Chelsea, iliyopo nafasi ya nne ikiikaribisha Swansea City na
Everton, inayoshika nafasi ya tano itakuwa ikicheza dhidi ya Sunderland ilihali watetezi Manchester United ikiifuata Hull City ugenini.
Kocha wa City, Manuel Pellegrini amesisitiza kwamba staili ya timu yao haitabadilika hata kama watakutana na timu inayoweza kwenda sambamba na mbinu zao, wao wanachotaka ni kuendelea kufunga mabao mengi, huku kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anaamini vijana wake hawatamuangusha mechi hiyo ya ugenini akimtegemea nahodha wake Luis Suarez anayeongoza kwa ufungaji kwa sasa katika ligi akiwa na mabao 19.
Ratiba kamili ya mechi za leo za EPL ni;
Hull City v Man Utd (saa 9:45)
Aston Villa v Crystal Palace (saa 12:00)
Cardiff City v Southampton (saa 12:00)
Chelsea v Swansea City (saa 12:00)
Everton v Sunderland (saa 12:00)
Newcastle Utd v Stoke City (saa 12:00)
Norwich City v Fulham (saa 12:00)
Tottenham Hotspur v West Bromwich (saa 12:00)
West Ham Utd v Arsenal (saa 12:00)
Man City v Liverpool (saa 2:30 usiku)


No comments:

Post a Comment