STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 12, 2014

Chelsea yabanwa yaweka rehani kiti cha uongozi EPL

West Brom striker Victor Anichebe scores against Chelsea
Victor Anichebe akifunga  bao la kusawazisha lililoinyima Chelsea ushindi
NAFASI ya Chelsea kuendelea kukalia kiti cha uongozi inategemea na matokeo ya mechi za leo za Ligi Kuu ya England baada ya timu hiyo kulazimishwa sare ya 1-1 ugenini dhidi ya West Bromwich.
Bao la 'jioni' lililofungwa na Victor Anichebe lilizima ndoto za Chelsea kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya Branislav Ivanovic kuandika  bao la kuongoza dakika tatu za nyongeza kabla ya mapumziko.
Kwa sare hiyo Chelsea imefikisha pointi 57 zinaweza kufikiwa na kupitwa na Arsenal na Manchester City ambazo zitakuwa dimbani usiku wa leo katika mfululizo wa ligi hiyo.
Arsenal waliokuwa wakiongoza ligi hiyo kwa muda mrefu waliocharazwa kwa aibu na Liverpool mwishoni mwa wiki itashuka dimbani leo uwanjwa wake wa nyumbani dhidi ya Manchester Utd.
Manchester City waliopo nafasi ya tatu wakiwa na pointio 54 itakuwa uwanja wake wa nyumbani wa Itihad kuikaribisha Sunderland.
Katika mechi nyingine zilizochezwa jana usiku zimeshuhudia Cardiff City na Aston Villa zikitoka suluhu ya bila kufungana, Hull City ikinyukwa nyumbani bao 1-0 na Southampton na West Ham United kushinda 2-0 dhidi ya  Norwich City.
Ligi hiyo itaendelea tena leo mbali na mechi mbili za Arsenal na Manchester Utd na Manchester City  dhidi ya Sunderland, pia leo kuna mechi za Stoke City dhidi ya Swansea City, Everton vs Crystal Palace, Newcastle United dhidi ya Tottenham Hotspur na Fulham itaikaribisha Liverpool.

No comments:

Post a Comment