STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 2, 2014

Tiketi za Elektroniki zaichanganya TFF. sasa yataka kikao cha dharura

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, limeagiza kifanyike kikao cha dharura kati ya Sekretarieti ya TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na benki ya CRDB ili kutathimini maendeleo ya matumizi ya tiketi za elektroniki.
Lengo la kikao hicho ni kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki ni kutafuta ufumbuzi pamoja changamoto zake.
Viwanja vinane nchini vimefungwa mfumo huo wa tiketi za elektroniki. Viwanja hivyo ni Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Uwanja wa Kaitaba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Uwanja wa Mkwakwani, na CCM Kirumba.
Katika hatua nyingine, TFF imeiagiza Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ifanyie marejeo (review) uamuzi wake wa kuagiza mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) irudiwe mkoani Tabora.
Maagizo hayo yametolewa na Kamati ya Utendaji iliyokutana jana (Februari 1 mwaka huu) baada ya kupokea vielelezo vipya kuhusiana na mechi hiyo iliyochezwa Novemba 22 mwaka jana mjini Shinyanga.
Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ilivunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya kupigwa na wachezaji wa Kanembwa JKT.
Pia Kamati ya Nidhamu ya TFF inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili tukio hilo la Shinyanga wakiwemo wachezaji wanane wa Kanembwa JKT waliripotiwa kumpiga mwamuzi wa mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment