Messi akishangilia moja ya mabao yake matatu alipoiangamiza Real Madrid |
Real Madrid wakishangilia moja ya mabao yao |
KLABU ya Real Madrid usiku wa kuamkia leo imechezea kichapo cha mabao 4-3 toka kwa wapinzani wa jadi Barcelona na kutoa baraka kwa mahasimu wao wa jiji la Madrid, Atletico Madrid kukikalia jumla kiti cha uongozi wa Ligi Kuu ya Hispania.
Mshambuliaji nyota wa Argentina, Lionel Messi alidhihirisha yeye ni bora baada ya kufunga hat trick kwenye pambano hilo lililochezwa uwanja wa Santiago Bernabeu, mjini Madrid.
Wageni walianza kuandika bao dakika ya saba kupitia kwa Andres Iniesta kabla ya Mfaransa, Karim Benzema kusawazisha bao hilo dakika ya 20 na kuongeza jingine la pili dakika ya 24.
Dakika tatu kabla ya mapumziko Messi aliisawazishia bao na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Kipindi kilipoanza iliwachukua wenyeji dakika 10 kuandika bao la tatu kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliyefunga kwa mkwaju wa penati.
Hata hivyo Lionel Messi alisawazisha hilo dakika ya 65 kwa mkwaju wa penati pia kabla ya kuongeza jingine dakika tano kabla ya pambano hilo kumalizika na kukamilisha hat trick yake na kuipa ushindi wa mabao 4-3 timu yake ya Barcelona.
Ushindi huo umeifanya Barcelona imeendelea kubakia nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 69, moja zaidi ya wapinzani wao Real Madrid na Atletico Madrid waliopo kileleni kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na matokeo baina yao wawili hao waliopo juu.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho Jumanne hadi Ijumaa kwa mechi ambazo zitaendelea kutoa taswira ya ubingwa wa nchi hiyi.
Jumanne;
Almería vs Real Sociedad
Málaga vs Espanyol
Jumatano:
Elche vs Athletic Club
Barcelona vs Celta de Vigo
Rayo Vallecano vs Osasuna
Alhamis:
Atlético Madrid vs Granada
Sevilla vs Real Madrid
Getafe vs Villarreal
Real Sociedad vs Real Valladolid
Ijumaa:
Levante vs Real Betis
Almería vs Valencia
No comments:
Post a Comment