STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 24, 2014

Tevez azidi kuipaisha Juve Italia, Milan yadroo

http://e2.365dm.com/14/03/660x350/Catania-v-Juventus-Carlos-Tevez-L-vies-with-C_3106513.jpg?20140323214233
Tevez akichuana na mchezaji wa Catania usiku wa jana kwenye Seria A
http://sport.bt.com/images/juve-grind-out-catania-win-136388712671108302?v=140323221505
Akishangilia bao lao

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Italia, Juventus imeendelea kutakata kwa kupata ushindi mwembamba ugenini dhidi ya Catania shukrani za pekee ziende kwa Carlos Teves aliyefunga bao hilo la pekee katika dakika ya 59.
Ushindi huo wa Juve umewafanya wafikishe jumla ya pointi 78 baada ya kucheza mechi 29 wakiiacha mbali Roma inayoshuka dimbani  kesho kuumana na Torino ikiwa na pointi zake 64.
Bao alilofunga Tevez nytota wa zamani wa Aston Villa, Manchester Utd na Manchester City, limemfanya afikishe jumla ya mabao 16 katika ligi hiyo na kulingana na nyota wa Torino, Ciro Immobile.
Katika mechi nyingine zilizochezwa usiku wa jana Napoli ilikubali kipigo kwenye uwanja wake wa nyumbani toka kwa Fiorentina, nazo timu za Lazio na AC Milan zikitoshana nguvu kwa kufunga bao 1-1, wanyeji wakijifunga kabla ya kusawazisha katika kipindi cha pili.
Kipute cha pili kinatarajiwa kuendea tena kesho kwa pambano la Roma itakayoikaribisha Torino, kabla ya keshokutwa Chievo kuumana na Bologna, Cagliari dhidi ya Hellas Verona, huku Genoa itaikaribisha Lazio na  Atalanta itaumana na Livorno.
Siku hiyo ya Jumatano pia kutakuw ana mechi nyingine ya kukata na shoka kati ya Fiorentina itakayoikaribisha Ac Milan, huku  Catania itaumana na Napoli, wakati  Juventus watakuwa nyumbani kuwakaribisha Parma na Sassuolo itakuwa mwenyeji wa Sampdoria.
Alhamis kutakuwa na pambano moja tu litakalowakutanisha Inter Milan ambayo jana ilichezea kichapo itakayoumana na Udinese.

No comments:

Post a Comment