WAKATI kasi ya wanawake
wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, imebainika kuwa asilimia 26.5 ya
wanawake nchini Tanzania wanafanya mapenzi kinyume na
maumbile.
Mfumo wa uzazi unaharibika; Watafiti wanabainisha kuwa kitendo
hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzaz.
Pia kina athari kubwa mno kwa mwanadamu, mojawapo ni ikiwemo uwezekano
mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna
vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya
kuambukiza vijidudu hivyo.
Mtafiti
Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alitoa ripoti hiyo hivi
karibuni hapa jijini Dar Es Salaam.
Mremi
akiwa na jopo la watafiti kutoka NIMR anasema kuwa wanawake hao
wamesema chanzo kikubwa kinachowapelekea kufanya ngono kinyume na
maumbile ni kujipatia kipato zaidi na Kuogopa kupata Mimba.
Vilevile
alizitaja sababu nyingine za wanawake kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni
kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya
makabila.
Sampuli
za utafiti Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es
salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha. Mremi anasema
“Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka
15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi,
wafanyakazi, wahudumu wa bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa
nyumbani Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume
ambao walihusishwa katika utafiti huo.
Imani
potofu kwa wanaume Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya
kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu
ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi kwa haraka
zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote.
Credit:E.Shiratu
No comments:
Post a Comment