MABINGWA wa zamani wa Afrika, TP Mazembe jana wamekumbana na kipigo cha mabao 2-1 katika pambano lao la mkondo wa kwanza wa hatia ya 16 Bora dhidi ya we nyeji wao, Sewe ya Ivory Coast.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta aliifungia timu yake bao la kufitia machozi baada ya wenyeji kujipatia mabao yake kupitia kwa Roger Assale katika dakika ya 38 kaba la kuongeza jingine kwa mkwaju wa penati dakika ya 82 kupitia Christian Kouame.
Hata hivyo wenyeji wakiamini wameisulubu Tp Mazembe kwa mabao mawili kavu, mtokea benchi Mbwana Samatta aliifunga bao la kufutia machozi ambalo linaweza kuwa msaada kwa vijana hao wa Lubumbashi kwa mechi ya mkondo wa pili wikiendi hii.
Samatta tegemeo la Taifa Stars na Mchezaji Bora wa Mazembe kwa msimu uliopita alifunga bao hilo dakika mbili kabla ya kumalizika kwa pambano hilo.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo ya Mabingwa Afrika, Horoya AC ya Guine ilikubali kichapo cha bao 1-0 kwa CS Sfaxien ya Tunisia, huku Cotonsport ya Cameroon ikidonyolewa kidude kimoja na ES Sétif ya Algeria wakiwa ugenini mjini Algers.
Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, CS Constatine ya Algeria imeizabua ASEC Memosa ya Ivory Coast kwa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment