STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 24, 2014

Golden Bush wachekelea kutoa mmoja timu ya taifa

http://1.bp.blogspot.com/-7rQ8msvfaDg/ULRXlG_surI/AAAAAAAADdo/3g-KgiVJ1F0/s640/Golden+Bush+FC+Logo.JPG
UONGOZI wa timu ya Golden Bush umesema umefurashwa na kitendo cha mmoja wa wachezaji wake wa timu ya vijana ya Golden Bush FC inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu Wilaya ya Kinondoni, Ayoub Lipati kuteuliwa kwenye timu ya Taifa ya Maboresho iliyotangazwa na TFF.
Lipati ambaye ni mashambuliaji ni mmoja wa wachezaji 36 walioteuliwa na jopo maalum la makocha 40 waliokuwa na kazi ya kusaka wachezaji kwa ajili ya kuboresha timu ya taifa, Taifa Stars katika kuelekea kwenye Fainali za Afrika 2015.
Mlezi wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' aliiambia MICHARAZO kuwa Golden Bush umejisikia faraja uteuzi wa Lipati kutokana na ukweli timu yao ndiyo kwanza ina miaka miwili tangu kuundwa kwake.
"Tumefurahia sana kufanikiwa kutoa mchezaji mmoja katika kikosi cha wachezaji 36 walioteuliwa na jopo maalum la kusaka vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars," alisema Ticotico.
Ticotico alisema imani yake Lipati atakuwa balozi mwema wa Golden Bush katika kikosi kinachotarajiwa kuingia kambini mjini Tukuyu Mbeya mapema mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment