STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 17, 2014

Waliopenya maboresho Taifa Stars kutajwa leo

Rais wa TFF, Jamal Malinzi
MCHAKATO wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, ulioshirikisha wang’amuzi wa vipaji zaidi ya 40 umekamilika jana na majina ya nyota hao yataanikwa kesho Jumatatu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, wachezaji hao watafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuingia kambini Tukuyu, Mbeya na watakaoingia kambini ni wale watakaokuwa wamefaulu vipimo.
Wang’amuzi wa vipaji waliokuwa Lushoto ni Abdul Mingange, Ayoub Nyenzi, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.
Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Kidao Wilfred, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Pelegrinius Rutayuga, Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward, Salum Madadi, Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.
Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred na Ayoub Nyenzi ambaye mbali ya kuwa  mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo, pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana.
Yumo pia Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi), Pelegrinius Rutayuga.
Mkakati huo umebuniwa na TFF kwa lengo la kupata nyota wa kujumuishwa katika kikosi cha sasa cha Stars inayokabliwa na kampeni ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.

No comments:

Post a Comment