TIMU
ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kucheza mechi
mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji Botswana na Lesotho kwa
ajili ya kujiandaa kuivaa Msumbiji (Mambas) imeelezwa jana jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa, alisema
kuwa tayari vyama vya soka vya nchi hizo mbili vimethibitisha kuwepo kwa
michezo hiyo itakayofanyika jijini Gaborone.
Mwesigwa
alisema kuwa Taifa Stars itaanza kuwakabili wenyeji Julai Mosi mwaka
huu na baadaye Julai 5 itashuka kucheza mechi ya pili kwa kuivaa timu ya
Taifa ya Lesotho.
Katibu
huyo wa zamani wa Yanga alisema kuwa maandalizi ya safari yamekamilika
na kikosi cha Stars kinatarajia kuondoka nchini leo saa 12:00 asubuhi
kuelekea Gaborone.
Alisema
kwamba nyota wote 26 waliotajwa wataondoka na wanaamini kambi hiyo
itasaidia kukiimarisha kikosi hicho kinachohitaji ushindi ili kiweze
kuingia hatua ya makundi.
Aliwataja
wachezaji watakaosafiri leo wakiwa chini ya Mholanzi, Mart Nooij, ni
pamoja na Deogratias Munishi 'Dida', Aishi Manula, Benedictor Tinoko,
Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub 'Cannavaro', Joram Nason,
Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato
Ngonyani.
Wachezaji
wengine ni Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said
Juma, Haroun Chanongo, Himid Mao, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin
Friday, Ramadhan Singano 'Messi', Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane
Yeya.
Mechi
ya kwanza kati ya Taifa Stars dhidi ya Mambas itakuwa kati ya Julai 19
na 20 na marudiano yatafanyika mjini Maputo baada ya wiki mbili.
Stars
ilifanikiwa kusonga mbele katika mashindano hayo ya kusaka tiketi ya
kucheza fainali za mwakani za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya
kuifunga Zimbabwe jumla ya magoli 3-2.
No comments:
Post a Comment