STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 26, 2014

26 waitwa Stars kuivaa MoroccoKOCHA mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Mart Nooirj ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kitakachocheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco.
Mechi hiyo, ambayo imo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), imepangwa kuchezwa Septemba 5 mwaka huu nchini Morocco.
Wachezaji wapya waliomo kwenye kikosi hicho ni kiungo Said Ndemla wa Simba SC na washambuliaji Mwagane Yeya wa Mbeya City na Juma Luizio wa ZESCO United ya Zambia.
Kikosi kamili ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Azam), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio ZESCO, Zambia).
Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment