STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 21, 2014

Snake Boy Jr, Nassib kurudiana Dar

Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli 
Na Mwandishi Wetu
 MABONDIA Nassibu Ramadhani pamoja na Mohamed Matumla 'Snake Boy Jr' wameingia makubaliano ya kuzipiga kwa mara ya pili siku ya septemba 27 katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es salaam.

Akizungumzia mpambano huo mratibu wake Yassin Abdallah 'Ustadhi' amesema mabondia hao wamekubaliana na kusaini mkataba wa kuzipiga siku hiyo, ambapo ni marudiano baina yao kwani walishakutana mapema mwaka huu na Matumla kumshinda mpinzani wake kwa pointi.

Ustaadh alisema siku ya pambano hilo ambalo ameshindwa kutabiri kama ni Nassib atalipa kisasi au Matumla kuendeleza ubabe kutakuwa na michezo kadhaa ya utangulizi.

Baadhi ya michezo hiyo ni pamoja na lile pambano la

  Issa Omardhidi ya Juma Fundi katika uzani wa kg 53 raundi nane, Sadiq Momba vs Tasha Mjuaji kg 59 raundi nane, huku Juma Mustafa atamkabili Bakari Dunda kg 61 raundi sita.

Pia siku hiyo wanadada Lulu  Kayage atapambana na Fatma Yazidu kg 51 raundi nne.

siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa  DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.

Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi

No comments:

Post a Comment