STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 21, 2014

Serikali kujenga kiwanda cha kuzalisha viua mbu

Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kutumia Euro Milioni 16 katika ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vinavyoua viluwiluwi vya mbu wanaoambukiza malaria ulioko chini ya shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Abel Ngapemba wakati wa mkutano nawaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
“Hivi sasa majengo yote yamekwisha kamilika katika eneo la Maili moja Kibaha Mkoani Pwani na mitambo yote imeshawasili na wataalamu wanaifunga ambapo kabla ya mwisho wa mwaka   uzalishaji  wa majaribio utaanza” Alisema Ngapemba.
Akifafanua zaidi Ngapemba alisema kiwanda hicho kitasaidia kuzalisha ajira  za moja kwa moja zipatazo 172 kwa watanzania.

Pia Ngapemba alibainisha kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni sita za viadudu kwa mwaka ambapo asilimia 80 ya dawa hizo zitatumika nchini na asilimia 20 zitauzwa nchi za nje ambazo tayari zimeonyesha nia ya kuzitaka dawa hizo.
Viadudu hivyo vinatengenezwa kutokana na vimelea ambao wanakuzwa kwa kutumia viinilishe mbalimbali na kunyinyiziwa katika maeneo yenye mazalia ya mbu ambapo viluwiluwi wa mbu wanapovila wanakufa
Kulingana na ripoti ya upembuzi yakinifu wa mradi huu uliofanywa na NDC kwa kushirikiana na kampuni ya Labiofam ya Cuba mwaka 2010, mbali na malaria kusababisha vifo vya Watanzania wapatao 80,000 kwa mwaka,ambapo watu milioni 18 huugua ugonjwa huo kila mwaka ambapo Serikali imekuwa ikitumia kiasi cha dola za marekani zipatazo milioni 240 kwa mwaka katika kupambana na ugonjwa huu.
Ujenzi wa Kiwanda hicho ulianza miaka miwili iliyopita na kuwekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete October mwaka 2013 lengo likiwa kupambana na hatimaye kutokomeza mbu wanaoeneza malaria na magonjwa mengine yaenezwayo na mbu.

No comments:

Post a Comment