STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, September 3, 2014

Azam, Yanga sasa kukipiga Sept 14 Ngao ya Hisani


Azam
Yanga
PAMBANO la kuwania Ngao ya Hisani kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania 2014-2015 uliokuwa ufanyike Septemba 13 kati ya mabingwa Azam na Yanga walioshika nafasi ya pili msimu uliopita utacheza siku ya Jumapili ya Septemba 14 imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, mchezo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa siku moja mbele tofauti na tarehe ya awali.
Mchezo huo utaambatana na shughuli za kijamii kama uchangiaji damu na maonyesho ya shughuli za wadau na maendeleo ya jamii Shirikisho la soka Tanzania (TFF) hutoa sehemu ya mapato ya mchezo huu kwa shirika/shughuli ya kijamii iliyochaguliwa kwa mwaka husika.
Yanga na Azam kwa sasa zipo kwenye maandalizi ya pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na ushindani ulioibuka baina ya timu hizo kwa siku za karibuni.

No comments:

Post a Comment