STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, September 3, 2014

Simba kuivaa Gor Mahia, APR Rwanda Dar

http://3.bp.blogspot.com/-GSCJMwiaYZs/UpCJnMip07I/AAAAAAAABZ0/vVHfo5FIxIE/s1600/simba+sc.JPGTIMU kongwe ya soka nchini, Simba mwishoni mwa wiki hii itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. 
Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo awali ilielezwa kuwa Simba ingecheza na Mtibwa Sugar kabla ya kuwepo kwa mabadiliko hayo. Taarifa toka ndani ya Simba zimesema maandalizi ya mechi hiyo yanaendelea vizuri, timu ikiwa kambini Zanzibar, chini ya Kocha wake mzoefu, Patrick Phiri kutoka Zambia. Kwa mujibu wa habari hizo, Simba huenda ikacheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa wiki ijayo kwa kumenyana na APR ya Rwanda. Mechi dhidi ya Gor Mahia itapigwa Jumamosi wakati mechi dhidi ya APR itapigwa Jumatano ijayo kwenye uwanja huo na ni maelekezo ya kocha Phiri.

No comments:

Post a Comment