STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, September 3, 2014

Ofisi ya Mkemia Mkuu yafichua siri nzito

https://2.bp.blogspot.com/-syyeXsLD9iE/VAWl9uREXOI/AAAAAAAAXks/rKiF1w4_3L4/s1600/Gloria%2BOmary.jpg
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai na Vinasaba Gloria Omar (kushoto) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. 
SULEIMAN MSUYAOFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema upungufu wa rasilimali watu, gharama kubwa za undeshaji, mchakato mrefu wa manunuzi ni baadhi ya changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili ofisi hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai na Vinasaba Gloria Omar wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Alisema changamoto nyingine ni uhitaji wa mitambo mipya inayoweza kubaini dawa za kulevya zenye mchanganyiko na kemikali bashirifu pamoja na matengenezo ya jingo la maabara ya uchunguzi wa makosa ya jinai.
Omar alisema iwapo changamoto hizo zitatatuliwa kwa wakati ofisi yao itaongeza tija katika ufanikishaji wa kazi zake kila siku kama ilivyo kuwa hapo awali.
Mkurugenzi huyo alisema baadhi ya mashine zina muda mrefu na pia zinauzwa bei kubwa ufinyu wa bajeti unakwamisha kununua zingine hali ambayo inasababisha kutoendana  na wakati kulingana na mabadiliko ya sampuli ambazo zinapatikana.
“ Ofisi yetu imepata mafanikio baadhi lakini changamoto ni kubwa kama nilivyozitaja hapo awali jambo ambalo kwa njia moja zinakwamisha malengo yetu” ,alisema.
Alitaja baadhi ya mafanikio ambayo yalipatikana  kwa kipindi cha mwaka 2013  ni Ofisi hiyo kuchunguza majalada 208, utoaji ushahidi mahakamani umeimarishwa na takwimu zimehuhishwa kwa kutumia mfumo wa komputa.
Mafanikio mengine ni kushirika maonyesho ya kimataifa yanayohusu uzuiwaji usafirishaji wa dawa za kulevya na kushiriki katika shughuli za kikosi kazi cha kupambana na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Mkurugenzi huyo wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai na Vinasaba alisema bajeti ya shilingi bilioni 1.4 imetengwa kwa ajili ya mitambo ya LCMS MS na GCMS MS kwa kipindi cha mwaka 2014/2015.
Aidha Omar alisema Ofisi ya Mkemia inapendekeza kuongezewa rasilimali watu pamoja na matumizi ya teknohama kwa kufanya mfumo mzima wa ununuzi, kutenga bajeti ya kotosha katika ofisi hiyo.
Mapendekezo mengine ni Serikali kuhakikisha kuwa inawapatia mashine za kisasa ambazo zitakuwa zikitoa majibu kulingana na wakati pamoja na mahitaji ya watu.
Kuhusiana na matokeo ya watu wanaopima vinasaba (DNA) kuonyesha asilimia 50 ya watu waliopima kuwa wanasingiziwa watoto alisema matokeo hayo ni sahihi jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa makini nini sababu yake.
Alisema kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kufanya vipimo anahitajika kufuata taratibu zote za kisheria pamoja na kulipa kiasi cha shilingi laki moja kwa kila sampuli moja.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment