STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, September 3, 2014

Yanga kujipima kwa Wakenya leo

Yanga
http://static.goal.com/258600/258645_heroa.jpg
Thika United
BAADA ya kupata ushindi katika mechi tatu mfululizo za kujipima nguvu dhidi ya timu za visiwani Zanzibar, Yanga ya kocha Marcio Maximo itakuwa kibaruani leo itakapowakabili Thika Utd ya Kenya.
Thika United inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, imeshatua jijini Dar tayari kwa mechi hiyo itakayokuwa ya kwanza ya kwanza ya kirafiki ya kimataifa kwa Maximo.

Pia ni mechi ya kwanza kwa Yanga na Maximo kucheza kwenye dimba la Taifa, litakalotumika kwa mchezo huo ambao mashabiki wangependa kuona vipaji vyao vipya vilivyosajiliwa na kukimbizwa Pemba kwenye kambi.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga wanaotarajiwa kuwa kivutio leo ni Geilson Santana 'Jaja' na ,Andrey Coutinho toka Brazil, Edward Charles na Said Juma waliosajiliwa hivi karibuni pamoja na vifaa vingine vya zamani.
Viingilio vya mchezo huo ni: VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/= Orange Tshs 10,000/=
Bluu & Kijani Tshs 5,000/= 

No comments:

Post a Comment