Allan Kamote (kulia) akionyeshana umwamba na Osgood Kayuni wa Malawi katika pambano lao la kuwania Mkanda wa Dunia wa UBO na Kamote kushinda kwa pointi. |
Thomas Mashali akimrushia konde Ramadhani Ali 'Alibaba' katika pambano lao lililochezwa jana kwenye uwanja wa Mkwakwani na Mashali kushindwa kwa TKO ya raundi ya tatu na kutwaa ubingwa wa UBO Afrika |
Kamote alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa UBO baada ya kumshinda kwa pointi bondia Osgood Kayuni kutoka Malawi katika pambano la raundi 12 la uzani wa Light.
Naye bondia Thomas Mashali alimchapa kwa TKO ya raundi ya tatu Mtanzania mwenzake Ramadhani Ali 'Alibaba' na kutwaa mkanda wa UBO Afrika katika pambano lao la raundi 10 na uzito wa kati. Michezo hiyo iliratibiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) na ilishuhudiwa pia Francis Miyeyusho akimshinda kwa pointi bondia wa Tanzania anayeishi Kenya Emilio Norfat.
Bondia Kamote licha ya kufanikiwa kutwaa mkanda huo wa Dunia wa UBO, lakini pia amefanikiwa kulipa kisasi kwa mpinzani wake kutoka Malawi aliyewahi kupigana naye mara mbili na kupigwa.
Katika pambano hilo mabondia wote walikuwa wakiviziana na kutupiana makonde kwa ufundi, hali ambayo iliwafanya mashabiki kuwa roho juu kwa kutojua nani atakayeibuka na ushindi hadi jaji alipotangaza matokeo yaliyompa ushindi Kamote.
Katika mechi nyingine za utangulizi, bondia Francis Miyeyusho alimshinda kwa pointi Emilio Norfat, huku Jacob Maganga na Said Mundi wakishindwa kutambiana kwa kutoka sare.
No comments:
Post a Comment