STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 2, 2014

Hatimaye Senzo Meyiwa akiwa kwa heshima zote Afrika Kusini

South African police officers salute the coffin of Senzo Meyiwa as thousands of members of the public watch the proceedings
Maafisa wa polisi nchini Afrika kusini wakipiga saluti jeneza la marehemu Senzo Meyiwa wakati umati wa wananchi wa Afrika kusini wakifuatilia.
Police officers place his coffin, draped in the South African national flag, at the centre of the pitch
Maafisa wa pilisi wakiwa wamebeba jeneza lililofunikwa kwa bendera ya taifa ya Afrika kusini katikati ya uwanja.
Meyiwa's widow Mandisa Meyiwa (right), his father Sam Meyiwa (second from left) and mother Ntombifuthi (third from lef, attend Senzo Meyiwa's funeral in Durban South Africa, Saturday, Nov. 1, 2014. Meyiwa, captain of the national soccer team was gunned down at his girlfriend's home, east of Johannesburg, last Sunday night. (AP Photo)
Pichani anaonekana mjane wa Meyiwa Mandisa Meyiwa (kulia), baba yake Sam (wapili kutoka kushoto) na mama yake Ntombifuthi (watatu kutoka kushoto)
Meyiwa, pictured playing for his country against Congo on October 15. The goalkeeper was adored by his teammates and fans
Meyiwa, akiwa katika picha wakati akiitumikia timu ya taifa dhidi ya Congo Oktoba 15. Mlinda mlango huyo ameagwa na wachezaji wenzake na mshabikiA picture taken in January 2013 shows South Africa President Jacob Zuma (left) posing with Senzo Meyiwa during his visit to the national team in Soweto

Picha iliyochukuliwa January 2013 ikionyesha Rais wa Afrika kusininPresident Jacob Zuma (kushoto) akipiga picha na Senzo Meyiwa wakati alipotembelea timu ya taifa mjini Soweto
Mjane wa Meyiwa
MAELFU ya waombolezaji waliofurika kwenye mazishi ya aliyekuwa Nahodha na Kipa tegemeo wa timu za Orlando Pirates na ile ya taifa, Bafana Bafana walionekana wakibubujikwa na machozi huku macho yao yakiwa na rangi nyekundu wakiwa wamevalia jezi nyeusi na wengine nyekundu wakisema buriani Senzo Meyiwa katika mji wa Durban.
Huzuni ilitawala watu wakilia kwa uchungu wakimlilia mlinda mlango huyo aliye uwawa akiwa na umri wa miaka 27 ambapo jeneza lake lilizungushwa uwanjani huku watu wakipuliza vuvuzela na kuimba nyimbo za kisoka.
Wengi waliohudhuria mazishi hayo waliungana kwa pamoja ndani ya uwanja wa Moses Mabhida akiwemo mjane wa Meyiwa, wanasiasa,wachezaji wa mpira wa miguu, watu mashuhuri na maarufu na kutoa salamu zao za mwisho kwa mpendwa wao.
Meyiwa, alipigwa risasi Jumapili iliyopita, baada ya majambazi kuingia nyumbani mwa mpenzi wake karibu na Johannesburg.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alifikishwa mahakamani Ijumaa na alishitakiwa kwa mauaji dhidi ya mlinda mlango huyo maarufu nchini Afrika Kusini.
Kifo cha Meyiwa kilisababisha mshituko mkubwa nchini Afrika Kusini na yameonyesha kiwango cha juu cha uahlifu wa kutumia nguvu nchini humo.
Mazishi yanafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Moses Mabhida Stadium katika mji wa Durban nyumbani kwa Meyiwa.
Senzo Meyiwa alionekana kama kivutio katika mchezo wa mpira miongoni mwa wananchi wa Afrika Kusini.
Wengi wa waombolezaji wamevaa fulana zenye picha ya Meyiwa, mtu ambaye alikuwa kivutio kikubwa kimichezo.
Mazishi ya mwanamichezo mwingine shujaa wa Afrika Kusini, bingwa wa zamani wa dunia wa mbio za mita 800 Mbulaeni Mulaudzi, pia yatafanyika Jumamosi.
Mulaudzi aliuawa katika ajali ya gari kabla ya kifo cha Meyiwa.
Rais Zuma ameamuru bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti siku ya Jumamosi ili kumuenzi mlinda mlango huyo wa timu ya taifa.
Mechi kati ya timu za Orlando Pirates na Kaiser Chiefs katika ligi ya Afrika Kusini imeahirishwa baada ya kifo cha Meyiwa.
Senzo Meyiwa alikuwa nahodha na mlinda mlango wa timu ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.
Mamlaka ya soka nchini humo wametangaza mchezo wa timu ya taifa ya Afrika Kusini wa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan ifanyike Durban.
Polisi wamesema Ijumaa kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya Meyiwa alitambuliwa katika gwaride la utambuzi.
Mtuhumiwa huyo, Zanokuhle Mbatha, mwenye umri wa miaka 25, anakabiliwa na mashitaka ya mauaji na ujambazi wa kutumia silaha na anatarajiwa kufikishwa tena mbele ya mahakama Novemba 11.Polisi wametangaza zawadi kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa zaidi kuhusu shambulio hilo ili kuwanasa watuhumiwa wengine.
Meyiwa alipigwa risasi akiwa nyumbani kwa mchumba wake huko kusini mashariki ya jiji la Johannesburg Jumapili iliyopita
Mwanamke akibubujikwa na machozi wakati wa sherehe ya kuuaga mwili wa mpendwa wao Meyiwa.

No comments:

Post a Comment