STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 2, 2014

Barcelona yapigwa kidude nyumbani na Celta Virgo


Celta Vigo goal
Wachezaji wa Celta Vigo wakishangilia bao pekee dhidi ya Barca
Neymar
Neymar licha ya kukukuruka kutaka kuendeleza rekodi ya mabao Barca alikwama jana kwa Celta Vigo
Lionel Messi
Messi akisikitika baada ya kukosa bao
BAO pekee lililofungwa dakika ya 55 na Joaquín Larrivey wa Celta Virgo lilitosha kuizamisha Barceona ikiwa nyumbani kwao katika pambano la La Liga lililochezwa uwanja wa Camp Nou.
Barcelona ikiwa na kikosi chake kamili walishindwa kuhimili vishindo vya wageni wao na kulala huku nyota wake Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar wakikosa mabao mengi ya wazi wakiwa lango la wpainzani wao ambao ushindi huo nui wa kwanza kwao kenye uwanja wa Camp Nou.
Kocha Luis Enrique amekuwa akitumia mfumo wa kuwachezesha kwa pamoja washambuliaji hao watatu kwa imani ya kuifanya timu yake itishe, lakini bado mfumo huo haujazaa matunda kwani wiki iliyopita walikumbana na kipigo cha mabao 3-1 kwa Real madrid katika pambano la El Classico mjini Madrid.

Kwa kipigo hicho imeifanya Barcelona kuporomoka hadi nafasi ya tatu ikiachia usukani wa ligi mikononi mwa wapinzani wao Real Madrid yenye pointi 24 na mabingwa watetezi Atletico Madrid waliopo wa pili na pointi 23, moja zaidi ya ilizonazo wakali hao wa 'Cataluna',
Barca wana hatihati ya kuporomoka zaidi iwapo Sevilla itakayokuwa ugenini leo itashinda mechi yake dhidi ya Athletic Bilbao kwani zinalinda pointi 22, ila wenzao wana mchezo mmoja mkononi ambao unachezwa leo ambapo kama itashinda itakwea hadi kileleni ikiiengua Real Madrid.

Celta Vigo goal
Celta Vigo scored with one of only four attempts on target to win the match
Neymar
Brazil striker Neymar could not add to his record of 11 goals in all competitions for Barcelona this season
Lionel Messi
Barcelona's Lionel Messi remains on 250 La Liga goals, one behind Telmo Zarra's all-time record

No comments:

Post a Comment