STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 2, 2014

Kombe la Chalenji lakwama Ethiopia, sasa huhamishiwa Sudan

RAIS wa CECAFA, Leodgar Tenga akiwa na Katibu wake, Nicolaus Musonye
Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati (CECAFA) kwa sasa linaangalia uwezekano wa kupata muandaaji mpya wa michuano ya mwaka huu 2014 ya chalenji kufuatia Ethiopia kujitoa.
Katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amenukuliwa toka Nairobi, Kenya kuwa Ethiopia imejitoa kuandaa michuano hiyo.
“Ethiopia imetuandikia na kusema hawako katika nafasi ya kuandaa michuano hiyo,” Musonye amesema na kuongeza kuwa CECAFA imekubali kujitoa kwao
“Hatuna la kufanya zaidi ya kukubali ombi la lakini tayari tumeanza kazi ya kusaka mwenyeji mpya.”
Musonye amethibtisha hilo licha ya shirikisho la soka la Ethiopia EFF kuwaandikia wakiwa wamechelewa, lakini amesema kuwa michuano hiyo itafanyika kwa tarehe iliyotajwa kati ya Novemba na Desemba na kwamba mwenyeji mpya atatangazwa wiki iyayo.
"Sudan yuko tayari akingojea hivyo michuano inaweza kuelekea Khartoum, lakini tutatangaza baadaye wiki ijayo"
Mwaka uliopita 2013 michuano hiyo ilifanyika nchini Kenya ambapo wenyeji walitwaa taji hilo baada ya kuifunga Sudan katika mchezo wa fainali uliopigwa katika dimba la Nyayo jijini Nairobi.

No comments:

Post a Comment