STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 3, 2014

Aguero awaliza Mashetani Wekundu, Spurs yaizima Aston Villa

Ilikuwa ikionekana ni ngumu leo kumfunga David de Gea. Kwa upande wake Sergio Aguero haikuwa hivyo kwani alidhihirisha kuwa yeye ni noma alipoifungia bao pekee kwa timu yake na kuipa ushindi City dhidi ya United.
Tayari dakika 63 zilikwisha kupita wakati Aguero akifunga goli hilo na kudhihirisha kuwa yeye ndiye shujaa wa 'derby' ya Manchester hii leo.
Wasiwasi ulitanda tangu mapema kufuatia United kupungua na kusali kumi kunako dakika ya 39 wakati Chris Smalling alipoondoshwa uwanjani na mwamuzi kwa makosa mawili huku pia Marcos Rojo akiumia bega.
Wakati huo Tottenham Hotspur ilitoka nyuma na kuizima Aston Villa kwa mabao 2-1 katika pambano la ugenini.
Spurs ilitanguliwa kufungwa bao la kipindi cha kwanza na wenyeji kupitia Weimann kabla ya Chadli kusawazisha dakika ya 84 na Harry Kane kufunga bao lake la saba katika mechi saba za Spurs na kuipa ushindi timu yake.
Katika pambano hilo wenyeji walimpoteza nyota wa Christian Benteke aliyelimwa kadi nyekundu dakika ya 65.
Sergio Aguero converts Gael Clichy's low cross from the left to put Manchester City 1-0 ahead in the Manchester derby
Sergio Aguero akiunganisha krosi ya Gael Clichy kutoka kushoto na kuwapa uongozi Manchester City wa bao 1-0 dhidi ya majirani zao Manchester United
Juhudi za Aguero zikionekana katika picha akipiga mpira unaomzidi David de Gea kunako dakika ya 63 uwanja wa Etihad
Aguero (third from left) is mobbed by his team-mates after giving Manchester City the lead against their local rivals United
United players (from left to right) Paddy McNair, Wayne Rooney and Luke Shaw appear dejected following City's goal

No comments:

Post a Comment