STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 3, 2014

Bale arejea dimbani Madrid ikiikaribisha Liverpool kesho Ulaya

Gareth Bale akiwa mazoezini
KLABU ya Real Madrid inayojiandaa kurudiana na Liverpool katika Ligi ya Mabingwa Ulaya imeongezewa nguvu baada ya nyota wake Gareth Bale kuanza mazoezi na wenzake.
Bale aliyekuwa majeruhi alikuwa akifanya mazoezi ya kujitegemea kabla ya jana kuanza kufanya pamoja na wenzake.
Bale raia wa Wales ni mmoja wa washambuliaji nyota na hatari wa kikosi cha Madrid.
Vinara hao wa La Liga itarudiana na Liverpool kesho mjini Madrid baada ya kuwanyoosha kwa mabao 3-0 katika mechi yao iliyopita kwenye uwanja wao wa Anfield.
Mechi nyingine za kesho ni Kundi A litashuhudia Juventus ikiumana na Olympiakos mjini Turin, Italia wakati Malmo itajiuliza upya kwa Atletico Madrid wakiwa kwao Sweden.
Kundi B mbali na Real Madrid na Liverpool kuwa kesho kutakuwa na mtanange kati ya  Basel dhidi ya  Ludogorets wakati Kundi C litashuhudia timu za Zenit ikiumana na Bayer Leverkusen na Benfica kuikaribisha Monaco.
Michezo mingine ni ile ya kundi D kati ya Arsenal dhidi ya Anderlecht na Borussia Dortmund ambayo inachechemea katika Bundesliga, itapoialika Galatasaray.

No comments:

Post a Comment