STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 3, 2014

Mart Nooij kutaja kikosi cha Stars cha kuifuata Swaziland

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/08/DSCN2670.jpg
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij
 KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.
Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.
Mwezi uliopita Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Benin na kuicharaza mabao 4-1 ikiwa ni wiki chache tangu wakung'utwe mabao 2-0 na Burundi mjini Bunjumbura.

No comments:

Post a Comment