STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 3, 2014

Mbeya City majanga, Mgambo JKT yatuma salam Jangwani


Mbeya City walipopigwa Mkwakwani jioni ya leo
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/05/273f8-63.jpg
Mgambo JKT iliyotuma salamu Jangwani
TIMU ya soka ya Mbeya City imeendelea kupata majanga baada ya jioni ya leo kutandikwa mabao 2-1 na Mgambo JKT katika pambano la kiporo cha Ligi Kuu Tanzania Bara lililokwama kuchezwa jana kwa sababu ya mvua kubwa iliyonyesha jijini Tanga.
Mbeya City ambayo ilikuwa inauguza kipigo toka kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Azam ilijikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma kwa mabao 2-0. 
Mabao yaliyofungwa na Malimi Busungu kwa mkwaju wa Penati dakika ya 11 na Ally Nassor kuongeza la pili dakika ya 24 kabla ya Steven Mazanda kuwapa Mbeya bao la kufutia machozi dakika ya 76.
Ushindi huo imeifanya Mgambo kufikisha jumla ya pointi 9 wakati Mbeya City imesalia mkiani ikiwa na pointi 5.
Mgambo JKT inajiandaa kufunga safari kuja Dar kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Yanga litakalopigwa siku ya Jumamosi.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA
                               P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01. Mtibwa Sugar    06  04  02  00  09  02  07   14
02.  Coastal Union   06  03  02   01  08   05 03  11
03.  Azam               06  03  01  02  06  03  03   10
04. Yanga               06  03  01  02  07   05  02  10
05. Kagera Sugar    06  02  03   01  05   03 02   09
06.  Mgambo JKT    06  03  00  03   04    05  -1  09
07. JKT Ruvu          06  02  01  03   05   07   -2  07
08. Ruvu Shooting  06  02  01   03  04   06   -2  07
09. Prisons             06  01  03   02  06   06  00   06
10. Simba              06  00  06   00  06    06  00  06
11. Ndanda Fc        06  02  00   04  08    10  -2  06
12. Polisi Moro       06  01  03  02   05    07   -2  06
13. Stand Utd         06  01  03   02  04   09  -5   06
14. Mbeya City       06   01  02   03  02   05  -3   05

No comments:

Post a Comment