STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 3, 2014

Majeruhi wazidi kumchanganya kocha Luis Van Gaal

http://www.nerdoholic.com/wp-content/uploads/2014/07/Van-Gaalmoyes1.jpg
Kocha Luis Van Gaal
KOCHA Louis Van Gaal wa Manchester United, yupo katika hali tete kufuatia timu yake kukumbwa na balaa la kuwakosa nyota wake tegemeo kutokana na kuwa majeruhi.
Jumla ya wachezaji nane wa Mashetani Wekundu ambao jana walilala ugenini bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao Manchester Citym, wapo nje ya dimba  wakiuguza majeraha mbalimbali japo baadhi wakitarajiwa pengine kurudi uwanjani wiki hii.
Radamel Falcao ana jeraha la sehemu ya nyuma 'kigimbi' ya mguu wake wa kulia
Falcao anauguza 'Kigimbi'
Moja ya wachezaji waliokosa mechi mbili zilizopita ni mshambuliaji Radamel Falcao ambaye aliumia sehemu ya nyuma ya mguu wake ambayo inafahamika kama kigimbi au Calf kwa jina la kitaalamu na anatarajiwa kurudi uwanjani tarehe 8 ya mwezi huu .
Marcos Rojo aliteguka bega kwenye mchezo dhidi ya Manchester City.
Marcos Rojo yeye katenguka bega jana wakati wakiumana na Man City
Marcos Rojo akitolewa uwanjani baada ya kuumia bega .
Mlinzi wa kimataifa wa Argentina Marcos Rojo ni jina lingine ambalo limeingia kwenye orodha ya majeruhi wa United baada ya kuteguka bega kwenye mchezo dhidi ya Manchester City .
Bado haijafahamika beki huyo atarudi lini uwanjani lakini hatarajiwi kuonekana kwa angalau siku 21 ambazo ni sawa na wiki tatu ambazo atalazimika kuwa nje ya uwanja .
Jonny Evans naye amekuwa nje kwa jeraha la kifundo cha mguu .
Jonny Evance naye yupo Wodi ya Majeruhi Old Trafford
Beki wa Ireland ya Kaskazini Jonny Evans naye ni miongoni mwa ‘wagonjwa ‘ walioko kwenye wodi ya Manchester United tangu alipoumia ‘enka’ takribani wiki tatu zilizopita .
Beki huyu anakaribia kurudi uwanjani na tarehe aliyopangiwa kuanza mazoezi mepesi ni mwishoni mwa wiki hii .
Phil Jones ana jeraha la ugoko alilopata kwenye mechi dhidi ya Chelsea.
Phil Jones anauguza ugoko
Majeruhi mwingine ni Phil Jones ambaye alipata jeraha kwenye eneo la ugoko kwenye mchezo ambao United ilicheza dhidi ya Chelsea na bado hajapangiwa tarehe ya kurudi uwanjani .
Rafael Da Silva
Rafael Da Silva

Jesse Lingard aliumia goti kwneye mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Swansea City.
Jesse Lingard anauguza goti kwa muda mrefu
Ashley Young ana jeraha la paja.
Ashley Young anaugulia maumivu ya paja

Kwa jumla United ina wachezaji saba wa kikosi chake cha kwanza ambao wako nje wakiuguza majeraha mbalimbali japo orodha hiyo inategemea kushuka na kufikia wachezaji watano baada ya kurejea uwanjani kwa Radamel Falcao na Jonny Evans huku Rafael Da Silva naye akiwa hayuko mbali kwani jeraha alilopata kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Manchester City sio kubwa hivyo huenda akampa afueni LVG.

No comments:

Post a Comment