STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, November 7, 2014

Simba wamcharukia Malinzi, waapa kufa na Dk Ndumbaro

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/05/kiki.jpg
Rais wa Simba Evance Aveva (kulia)
http://3.bp.blogspot.com/-7SaTPFyosgw/U57DZy72fDI/AAAAAAAFq9g/qIuuv5oLj7g/s1600/3.jpg
Dk Ndumbaro (kulia)
UONGOZI wa Klabu ya Simba umelivaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu kauli yao ya kuzitaka klabu kutojihusisha na wakili wa kujitegemea Damas Ndumbaro kupitia kampuni yake ya Maleta & Ndumbaro Advocate.
Rais wa Simba, Evans Aveva, amefunguka kuwa kwa upande wao bado wanaendelea kumsapoti Ndumbaro kwa asilimia 100 kwa sababu wao ndiyo waliomtuma na kudai kuwa watashirikiana naye kama kawaida katika masuala ya soka.
“Kamati iliyoshughulikia suala hilo ni huru na kwa upande wetu Simba tupo mstari wa mbele kuhusu suala hilo na tunamsapoti.
“Tutaendelea kumtumia Ndumbaro kama kawaida kwani tunatetea haki yetu na tunapinga vikali makato ya asilimia tano ya mapato.
“Hakuna waraka wowote tuliopewa klabu kuhusu jambo hilo,” alisema Aveva.
TFF ilitangaza kumfungia Ndumbaro kujihusisha na soka kwa miaka saba kutokana na kile kilichoelezwa kukiuka kanuni kadhaa za shirikisho hilo.

SALEH JEMBE

No comments:

Post a Comment