STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 4, 2014

Dokii Hakuna Kama Mwanamke videoni


MSANII Ummy Wenceslaus 'Dokii' ameachia video ya wimbo wake mpya wa 'Hakuna Kama Mwanamke' huku akianza mchakato wa kutengenezea video ya wimbo wake mwingine uitwao 'Nampenda Dereva wa Bodaboda'.
Akizungumza na MICHARAZO, Dokii alisema video yake mpya imetengenezwa na Pablo ambaye pia ndiye aliyepewa jukumu la kuitengeneza video ya wimbo wa 'Nampenda Dereva wa Bodaboda'.
"Tayari nimeshaiachia video ya wimbo wangu wa 'Hakuna Kama Mwanamke' ambao 'audio' yake imetengenezwa studuio za Recho Records chini ya mtayarishaji aitwaye Shivo," alisema Dokii.
Alisema wimbo wake wa Nampenda Dereva wa Boda Boda' uliotengenezwa Akhenato Records chini ya Lil Ghetto, utaanza kurekodiwa video yake wiki ijayo kabla ya kuachiwa hewani.
"Video hiyo nayo itatengenezwa na Pablo, hivyo mashabiki wangu wajiandae kushuhudia kazi hiyo mapema kabla ya kumalizika kwa mwezi huu," alisema Dokii.
Muigizaji na mwanamitindo huyo alisema, ameamua kutoa kazi hizo mfululizo kuthibitisha alivyoelekeza nguvu zake katika fani ya muziki akiipa kisogo kwa muda kazi ya uigizaji filamu.

No comments:

Post a Comment